Zitto: Nimechoka Kuzushiwa na kuchafuliwa

Monday, November 11, 2013

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe
Na Agatha Charles, Tabora:    

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ameibuka na kutoa kauli na tamko dhidi ya tuhuma mpya dhidi yake zilizosambazwa katika mitandao ya intaneti katika siku za hivi karibuni.

Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Mjini, amefanya hivyo akitumia majukwaa mawili tofauti.

Mwanasiasa huyo kijana ambaye amejipambanua kuwa mtetezi wa misingi ya utaifa, raslimali za nchi, uchumi na masuala ya utawala bora ndani na nje ya chama chake, alifanya hivyo kwa mara ya kwanza juzi jioni, wakati alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilayani Kariua, Mkoa wa Tabora.

“Katika umri huu mdogo, nimepigwa mishale mingi ya kisiasa, mimi ni binadamu nina damu, nikipigwa hii mishale damu inatoka, ninaumia, sasa nimechoka kupigwa mishale, lazima sasa tuambiane ukweli,” alisema Zitto.

Saa kadhaa baada ya hotuba yake hiyo, Zitto ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa katika mzozo wa wazi na baadhi ya viongozi wenzake ndani ya Chadema, alisambaza tamko la maandishi ambalo lilibeba ujumbe unaofanana na ule alioutoa Kariua.

Awali katika mkutano wa Kariua, Zitto alisema alikuwa hayuko tayari kuendelea kukaa kimya pasipo kuchukua hatua zikiwamo za kisheria wakati akichafuliwa.

Alisema alikuwa ameshamwandikia barua Katibu Mkuu wake, Dk. Wilibrod Slaa, akihoji iwapo taarifa ya kumchafua iliyosambazwa katika mitandao ya intaneti chini ya kiichwa cha habari kisemacho “Taarifa ya Siri ya Chadema” ni ya chama hicho au la.

Zitto aliyekuwa akizungumzia matokeo ya ziara yake ya kufuatilia kuhusu fedha zilizofichwa na baadhi ya Watanzania katika mabenki ya Uswisi na kwingineko Ulaya, alieleza kusikitishwa na kile alichodai kuwa ni kikundi cha watu ndani ya Chadema ambacho kimekuwa mstari wa mbele kumpaka matope.

“Wakati nafanya kazi hii ya hatari ya kufuatilia hizo fedha zilizofichwa nje ya nchi, navunjwa nguvu na watu ambao tuko chama kimoja kwani imekuwa ni kawaida unapofanya siasa, lazima upate mashambulizi na sasa nashambuliwa na chama changu.

“Katika hali ya kawaida, wenzagu tulionao katika chama ndio waliopaswa kunipa nguvu, kwani tuna kazi kubwa ya kupambana na ‘lidude likubwa linaloitwa CCM,” alisema Zitto.

Akifafanua na pasipo kutaja jina la mtu, alisema kuna watu wachache ambao hawana kazi ndani ya chama hicho ambao shughuli yao imekuwa ni kugonganisha viongozi ili wagombane.

Akirejea historia ya kuchafuliwa kwake, Zitto alisema hali hiyo ilianza mwaka 2009 baada ya kujitokeza na kugombea uenyekiti wa taifa wa Chadema akichuana na Freeman Mbowe.

Alieleza kushangazwa na hali hiyo ambayo alisema inakinzana na kile kilichotokea mwaka 1995 wakati waasisi wawili wa Chadema, Edwin Mtei na Bob Makani walipojitokeza kusaka uteuzi wa mtu ambaye angekiwasilisha chama hicho katika kugombea urais.

Alisema mara baada ya mmoja wao kupitishwa na chama chao, makundi yote yaliyotokana na harakati hizo yalivunjwa na chama kikaendelea kubakia kimoja.

“Mwaka 2009, niliamua kugombea uenyekiti kwa sababu nilijua katika chama chetu kuna demokrasia inayomruhusu kila mmoja kugombea nafasi anayoona inamfaa. Lakini, kitendo cha mimi kugombea kikaonekana ni nongwa japokuwa wapo wengine waliogombea mwaka 1998 na hakukuwa na migogoro.

“Sasa, watu wanaona uchaguzi (ndani ya Chadema) unakaribia, vurugu na ugomvi vinaanza bila sababu yoyote. Lakini, kwa mtu kama mimi niliyeingia kwenye siasa nikiwa mdogo, najua tumefanya mengi na tumeibua mambo mengi pia,” alisema akijigamba.

Katika taarifa yake ya maandishi aliyoisambaza jana, Zitto aligusia kwa muhtasari kuhusu tuhuma kadha wa kadha ambazo ndizo zilizosababisha aandike barua kwa Dk. Slaa.

“Nilipokuwa katika ziara ya Bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu, nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa Taarifa ya siri ya Chadema ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

“Taarifa ya Chadema inasema Chadema kimekuwa kikichunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka CCM ili kuivuruga Chadema.

“Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes, ambaye kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola za Marekani 250,000 kupitia kwenye akaunti yake binafsi,” alisema Zitto.

Katika tamko lake hilo, Zitto aliita taarifa hiyo iliyojaa mambo mengi ya kimaadili, kuwa ni ya “kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha”

Mbali ya hilo, Zitto alieleza kusikitishwa, kukasirishwa na kufedheheshwa na taarifa hiyo ambayo alisema ilikuwa ikilenga kumtoa katika nia yake ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao.

Kutokana na hali hiyo, Zitto alisema hawezi kukubali watu watumie jina lake na uanasiasa wake kumchafua yeye na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.

Zitto katika taarifa yake hiyo alisema tayari raia wa Kijerumani aliyedaiwa kumfichia fedha alikuwa amekana tuhuma hizo kupitia maelezo alyoyatoa kwa viongozi wa Chadema.

Kama hiyo haitoshi, Zitto alieleza kukerwa pia na hatua ya ripoti hiyo kulitaja jina la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ikimhusisha na yeye kuficha fedha zinazomhusu yeye.

 “Niseme mapema, kwamba tangu kuzaliwa kwangu, sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama,” alieleza mwanasiasa huyo.

Akiendelea, Zitto alisema alikuwa amepokea taarifa za kutishiwa maisha na mtu aliyemtaja kwa jina la Theo Mutahaba ambaye pamoja na mambo mengine alimtaka aache kupambana na masuala ya ufisadi.

“Kwa maana hiyo, natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii, nitahakikisha wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.

“Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, “Struggle is my life,” alihitimisha Zitto taarifa yake hiyo.
Soma Habari Kamili | comments

Kenya yamuunga mkono JK

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Na Benjamin Masese, Dar es Salaam:    

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, ameipongeza Tanzania kwa hatua ya kutangaza kuwa haiko tayari kutoka katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kama ilivyodhaniwa hapo awali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema Kenya inaunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Novemba 7, mwaka huu kuwa haitajitoa na wala haitakuwa chanzo cha kuvunjika kwa EAC.

Alisema bila Tanzania hakuna Afrika Mashariki na bila Afrika Mashariki hakuna Tanzania.

“Kama unavyojua Kenya na Tanzania tumekuwa tukiijenga Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu, tuko na mafanikio mengi, kuna mambo mengi tumeyafanya, kuna njia ndefu imebakia na kuna mambo mengi yasiyoweza kupimwa kati ya nchi hizi.

“Tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashariki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na tuendelee kuwa hivyo,” alisema Amina.

Amina ambaye ametumwa na Rais Uhuru Kenyata kuja kutoa ujumbe huo, alisema ni vyema nchi hizo zikaendelea kushirikiana kwa kuwa zenyewe ni za kwanza kuunda umoja huo, hivyo ziendelee kuungana kwa ajili ya kuudumisha.

Alisema walikuwa na wasiwasi kuwa Tanzania ingejitoa kutoka EAC, kutokana na hali iliyojitokeza kwa baadhi ya nchi kuendesha mikutano yao bila kuishirikisha pamoja na Burundi.

Alisema kuwa hakuna namna ambavyo Tanzania na Kenya zitatenganishwa kwa namna ambavyo zimejenga muingiliano mkubwa wa kijamii na kiuchumi, huku akiomba Tanzania kuisaidia kusukuma ombi la Kenya la kutaka kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi kwa ajili ya kumpa fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, alisema Serikali yake imefurahi kuona Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza kwa kuinusuru EAC kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na si ya viongozi.

Aliahidi kushirikiana na Kenya katika masuala mbalimbali likiwamo la kutaka kesi inayomkabili Rais Kenyatta katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi.

Katika hatua nyingine, Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kamwe ushirikiano wa Kenya, Uganda na Rwanda wa kuzitenga Tanzania na Burundi katika mipango ya EAC usingedumu kwa sababu uongozi wao ni wa kidikteta.

Akizungumza Dar es Salaam jana juu ya hotuba ya Rais Kikwete kuhusu EAC, alisema chama hicho kinaunga mkono msimamo wa Tanzania.

Alisema CUF kinalaani vikali vitimbwi vilivyokuwa vikifanywa na Rais wa Rwanda, Kenya na Uganda na kuitenga Tanzania na Burundi na kuongeza kuna haja sasa ya kuwa na tahadhari na viongozi hao katika suala la usalama wa raia na nchi kwa ujumla.

Alisema ushirika wa nchi hizo na mipango yao iliyokuwa ikifanyika isingedumu, kwa sababu uongozi wa Uganda na Rwanda ni wa kidikteta huku Kenya haina umoja wa kitaifa kutokana na kugawanyika vipande viwili.

“Ninachomuomba Rais Kikwete watakapokutana wakuu wa nchi hizo awape vidonge vyao, najua mwezi huu Baraza la Mawaziri litawasilisha mapendekezo ya majadiliano ya mkutano wa 15 kwa wakuu wa nchi,” alisema na kuongeza:

“Tumesikia baada ya hotuba ya Rais Kikwete, wameanza kujing’atang’ata lakini walichokuwa wakifikiria kukifanya ni ndoto za mchana, mfano Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta tangu achaguliwe anasuasua kufanya mikutano upande wa upinzani wake na hilo limeifanya nchi kukosa umoja wa kitaifa.

“Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa mstari wa mbele kuharakisha kufikia Shirikisho la Kisiasa kwa lengo la kutaka kuwa Rais wa kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki.

“Shirikisho la kisiasa la Kenya, Uganda na Rwanda hizo ni ndoto na wanajifurahisha katika karne hii ya 21, shirikisho lazima lijikite katika mfumo wa demokrasia, Kenya imepiga hatua kubwa kujenga demokrasia lakini haijafanikiwa kujenga umoja wa kitaifa.

“Namuomba Rais Kikwete kuwa makini katika suala la soko la pamoja hasa katika ajira, ardhi na uhamiaji hivyo vitu visiingizwe katika soko la Afrika Mashariki bila kutafakari, Watanzania bado wamezubaa katika ardhi yao.

“Kuna jambo limejificha katika EAC, mimi nadhani ziara ya Rais Barack Obama kuja Tanzania ilielekea kutowafurahisha, ndio maana Kenya ilifikia hatua ya kususia mkutano wa wafanyabiashara wa Afrika ulioandaliwa na Corporate Council on Africa.

“Pia uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda umezorota baada ya Rais Kikwete kuwapa ushauri viongozi wenzake katika mkutano wa Umoja wa Afrika kwamba njia pekee ya kumaliza migogoro ya kisiasa na kuleta amani katika nchi za Kongo, Rwanda na Uganda ni kufanya mazungumzo mezani.

“Jambo jingine ni baada ya Tanzania kukubali kupeleka wanajeshi wake Kongo kama sehemu ya Jeshi la Umoja wa Mataifa kuleta amani mashariki ya Kongo, ambapo limesaidia kusambaratisha kundi la waasi wa M23.”
Soma Habari Kamili | comments

Uhaba wa chakula kuikumba mikoa 16

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Na Debora Sanja, Dodoma:  

HALMASHAURI 61 katika mikoa 16, zinatarajiwa kuwa na uhaba wa chakula.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni juzi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 13 wa Bunge.

Alisema halmashauri hizo zipo katika Mikoa ya Manyara, Shinyanga, Simiyu, Arusha, Dodoma, Lindi, Tanga, Singida, Mara, Morogoro, Kilimanjaro, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kigoma na Tabora.

Alizitaka halmashauri zinazohusika katika mikoa hiyo, kufuatilia kwa karibu utaratibu wa kupata chakula kinachotolewa kutoka maeneo yenye ziada.

Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa chakula hicho kinafika mapema katika maeneo yao kabla wananchi wa maeneo husika hawajaanza kulalamika.

“Kwa ujumla hali ya upatikanaji wa chakula nchini hadi kufikia Oktoba, 2013 ni ya kuridhisha kutokana na mavuno mazuri ya msimu wa kilimo wa mwaka 2012/2013, ambapo mazao yake yanaendelea kuingia sokoni kutoka maeneo mbalimbali nchini.

“Tathimini ya awali iliyofanyika Julai, mwaka huu inaonyesha kuwa uzalishaji wa chakula katika msimu wa kilimo wa mwaka 2012/2013, utafikia tani 14,383,845,” alisema Pinda.

Alisema kutokana na hali ya upatikanaji wa chakula kuwa nzuri, bei za wastani za vyakula hasa mahindi na mchele katika soko nchini zimeendelea kushuka.

Aidha, alisema Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), imepanga kununua tani 250,000 za nafaka katika msimu wa mwaka 2013/2014, hadi kufikia Oktoba 23, mwaka huu ulishanunua tani 218,412.

Aidha, alizungumzia mpango wa ruzuku za pembejeo, uzalishaji na ununuzi wa mazao ya biashara, operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo mbalimbali, hali ya ulinzi na usalama nchini na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Soma Habari Kamili | comments

Lowassa: Nasikitishwa elimu duni shule za kata

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam:   

WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, amesikitishwa na kiwango duni cha elimu katika shule za sekondari za kata na baadhi ya vyuo vya elimu ya juu.

Akizungumza katika harambee ya kuchangia mfuko wa elimu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, alisema kiwango cha elimu katika shule hizo kinamsikitisha kwa kuwa ni cha chini.

“Napenda niseme wazi kuwa kiwango cha elimu katika shule za kata na baadhi ya vyuo vikuu, kwa kweli ni vya chini, hili mimi linanisikitisha sana kwa sababu elimu bora ni mkombozi kwa mtoto wa Kitanzania,” alisema Lowassa.

Alipongeza kanisa kwa kusaidia juhudi za Serikali katika kuimarisha na kuboresha elimu, ambapo shule nyingi za kanisa zimekuwa na kiwango cha juu cha elimu.

Alitumia nafasi hiyo kuonyesha misuli yake kisiasa na kijamii ambayo ni marafiki wanaomsindikiza katika harambee mbalimbali.

“Sasa napenda Watanzania kupitia kwenu kuwaonyesha hawa marafiki zangu ambao wamekuwa wananisindikiza katika harambee, maana kumekuwa na maneno maneno,” alisema Lowassa baada ya wakili maarufu, Sadock Magai kuwasilisha michango ya marafiki.

Marafiki wa Lowassa walichangia Sh milioni 50 ambao ni Lawrence Masha, Innocent Macha, Bashir Awale, Hamis Kindoroko na Lemmy Bathelemew.

Aidha, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, alichangia Sh milioni tatu na Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azan, alichangia Sh milioni mbili.

“Nampongeza na kumshukuru Idd Azan kwa kuja kwake kunisindikiza na kuchangia, hii ndiyo Tanzania ninayoijua, isiyo na dini, watu wa dini zote mnashirikiana,” alisema Lowassa.

Katika harambee hiyo, jumla ya Sh milioni 615 zikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa ni Sh milioni 250.
Soma Habari Kamili | comments

Dk. Shein azitaka wizara kuzingatia vipaumbele

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein
Na Mwandishi Maalumu, Zanzibar:  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesisitiza umuhimu wa wizara na idara za Serikali kuzingatia vipaumbele katika kupanga mipango ya maendeleo ya kila mwaka.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akihitimisha Taarifa ya Thathimini ya Utekelezaji Kazi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 na robo mwaka wa mwaka wa fedha wa 2013-2014.

Alisema lengo la mikutano hiyo ni kufanya tathimini ya namna Serikali inavyotekeleza majukumu iliyojipangia kwa minajili ya kuzingatia na kuangalia utekelezaji wa bajeti na malengo yaliyowekwa.

“Dhamira yetu ni kujitathimini sisi wenyewe namna tunavyopanga na kutekeleza malengo tuliyojiwekea kwa kuangalia uwiano kati ya kiwango cha fedha kinachotolewa katika bajeti na kiwango cha utekelezaji wa malengo ya wizara na idara zake,” alisema Dk. Shein.

Alisisitiza umakini katika kuainisha na kupanga vipaumbele katika kila idara katika wizara kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji, ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa malengo ya mipango ya Serikali, huku dhamira kuu ikiwa ni kuongeza ufanisi na tija katika utendaji serikalini.

Akizungumzia kuhusu huduma za upimaji wa macho kwa watoto, aliitaka wizara kuweka mipango madhubuti ya namna ya kuwasaidia watoto ambao wanagundulika na matatizo ya macho, lakini wazazi wao hawana uwezo wa kugharimia matibabu.

Alishukuru mafanikio ya kitengo cha benki ya damu kwa kutimiza malengo ya mwaka uliopita kwa zaidi ya asilimia 100, lakini akahimiza kitengo hicho kujiwekea lengo la kujitegemea katika shughuli zake.

“Lengo letu liwe ni kujitegemea katika kuendesha benki ya damu na kwa kuanzia mwaka ujao wa fedha, kiwango cha fedha katika bajeti ya kitengo hicho kiongezwe hatua kwa hatua hadi kufikia kujitegemea kwa asilimia mia moja,” alisema Dk. Shein.

Alizungumzia umuhimu wa uwekaji wa takwimu sahihi katika sekta ya afya huku akihimiza ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na binafsi katika suala hilo.

“Kupata takwimu sahihi kitaifa hasa wakati wa magonjwa ya milipuko ni muhimu kuwapo na ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na binafsi,” alisema Dk. Shein.

Awali, Waziri wa Afya, Juma Duni Haji, alisema huduma za afya nchini zinazidi kuimairika kutokana na Serikali wakati wote kuwa sikivu kwa masuala ya afya.

Alisema wizara hiyo hivi sasa inakabiliana na tatizo la ongezeko la maombi kutoka kwa watumishi wa wizara hiyo kutaka kujiendeleza kimasomo, ikiwamo kozi mpya ya udaktari iliyoanzishwa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Saleh Jidawi, alisema katika mwaka wa fedha uliopita jumla ya wagonjwa wa macho 10,558 walichunguzwa na kupatiwa matibabu katika vituo vya afya 32 na vijiji 26 Unguja na Pemba.

Alisema uchunguzi wa macho ulifanyika katika shule 26 Unguja na Pemba, ambapo watoto 867 walipimwa macho miongoni mwao 278 walipatiwa miwani kwa kushirikiana na Kitengo cha Elimu Mjumuisho cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Kuhusu Mpango wa Damu Salama, alisema mpango huo uliweza kufikia lengo mwaka uliopita kwa asilimia 110 kutoka lengo la kukusanya damu lita 8,000 hadi lita 8,808.

Alisema hatua hiyo mbali ya kuwa ni mafanikio makubwa kwa kuvuka lengo, iliiwezesha Serikali kukidhi mahitaji ya damu kwa hospitali zote zinazotoa huduma hiyo nchini.
Soma Habari Kamili | comments

Haya weee mambo na yaje

Saturday, November 9, 2013

Bunge lacharuka Dodoma
TACLOBAN, Philippines (Reuters) - One of the strongest typhoons ever to make landfall devastated the central Philippines, killing more than 1,000 people in one city alone and 200 in another province, the Red Cross estimated on Saturday, as reports of high casualties began to emerge.

A day after Typhoon Haiyan churned through the Philippine archipelago in a straight line from east to west, rescue teams struggled to reach far-flung regions, hampered by washed out roads, many choked with debris and fallen trees.

The death toll is expected to rise sharply from the fast-moving storm, whose circumference eclipsed the whole country and which late on Saturday was heading for Vietnam.

Among the hardest hit was coastal Tacloban in central Leyte province, where preliminary estimates suggest more than 1,000 people were killed, said Gwendolyn Pang, secretary general of the Philippine Red Cross, as water surges rushed through the city.

"An estimated more than 1,000 bodies were seen floating in Tacloban as reported by our Red Cross teams," she told Reuters. "In Samar, about 200 deaths. Validation is ongoing."

She expected a more exact number to emerge after a more precise counting of bodies on the ground in those regions.

Witnesses said bodies covered in plastic were lying on the streets. Television footage shows cars piled atop each other.

"The last time I saw something of this scale was in the aftermath of the Indian Ocean Tsunami," said Sebastian Rhodes Stampa, head of the U.N. Disaster Assessment Coordination Team sent to Tacloban, referring to the 2004 earthquake and tsunami.

"This is destruction on a massive scale. There are cars thrown like tumbleweed and the streets are strewn with debris."

The category 5 "super typhoon" weakened to a category 4 on Saturday, though forecasters said it could strengthen again over the South China Sea en route to Vietnam.

Authorities in 15 provinces in Vietnam have started to call back boats and prepare for possible landslides. Nearly 300,000 people were moved to safer areas in two provinces alone - Da Nang and Quang Nam - according to the government's website.
Soma Habari Kamili | comments

Mambo mbamboa mamboyote

Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge
TACLOBAN, Philippines (Reuters) - One of the strongest typhoons ever to make landfall devastated the central Philippines, killing more than 1,000 people in one city alone and 200 in another province, the Red Cross estimated on Saturday, as reports of high casualties began to emerge.

A day after Typhoon Haiyan churned through the Philippine archipelago in a straight line from east to west, rescue teams struggled to reach far-flung regions, hampered by washed out roads, many choked with debris and fallen trees.

The death toll is expected to rise sharply from the fast-moving storm, whose circumference eclipsed the whole country and which late on Saturday was heading for Vietnam.

Among the hardest hit was coastal Tacloban in central Leyte province, where preliminary estimates suggest more than 1,000 people were killed, said Gwendolyn Pang, secretary general of the Philippine Red Cross, as water surges rushed through the city.

"An estimated more than 1,000 bodies were seen floating in Tacloban as reported by our Red Cross teams," she told Reuters. "In Samar, about 200 deaths. Validation is ongoing."

She expected a more exact number to emerge after a more precise counting of bodies on the ground in those regions.

Witnesses said bodies covered in plastic were lying on the streets. Television footage shows cars piled atop each other.

"The last time I saw something of this scale was in the aftermath of the Indian Ocean Tsunami," said Sebastian Rhodes Stampa, head of the U.N. Disaster Assessment Coordination Team sent to Tacloban, referring to the 2004 earthquake and tsunami.

"This is destruction on a massive scale. There are cars thrown like tumbleweed and the streets are strewn with debris."

The category 5 "super typhoon" weakened to a category 4 on Saturday, though forecasters said it could strengthen again over the South China Sea en route to Vietnam.

Authorities in 15 provinces in Vietnam have started to call back boats and prepare for possible landslides. Nearly 300,000 people were moved to safer areas in two provinces alone - Da Nang and Quang Nam - according to the government's website.
Soma Habari Kamili | comments

Michezo

Burudani

Habari za Kimataifa

Mawasiliano

Idadi ya waliotutembelea

Hifadhi ya Picha

Wafuatiliaji

Followers

Páginas

Powered by Blogger.

Subscribe

 
Support : Copyright © 2013. Gazeti la Rai - Haki zote zimehifadhiwa
Imewezeshwa na New Habari (2006) Ltd